诗篇 87

我的泉源都在你里面

Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 2Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. 3Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: 4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” 5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” 6Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” 7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

已复制!
Aa