Psalms 93

The Lord reigns, robed in majesty

Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa. 2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele. 3Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.

4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu. 5Ee Bwana, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.

Copied!
Aa