시편 120
내가 환난 중에 여호와께 부르짖었더니
Wimbo wa kwenda juu. Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu. 2Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu. 3Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. 5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari! 6Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.
복사됨!
Aa