Midvash

Romans 6:14-18

14Maana, dhambi haitawatawala ninyi tena, kwani hamko chini ya Sheria, bali chini ya neema.n

15Basi, tuseme nini? Je, tutende dhambi ati kwa sababu hatuko chini ya Sheria bali chini ya neema? Hata kidogo!o

16Mnajua kwamba mkijitolea ninyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo—au watumwa wa dhambi, na matokeo yake ni kifo, au wa utii, na matokeo yake ni kukubaliwa kuwa waadilifu.p

17Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini—namshukuru Mungu—mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.q

18Mlikombolewa kutoka utumwa wa dhambi, mkawa watumwa wa uadilifu.r

Copiado para área de transferência

Text Size

Aa

Reading Theme

Reading mode