Matthew 9:27-31
27Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, “Mwana wa Daudi, utuhurumie!”m
28Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, “Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?” Nao wakamjibu, “Naam, Mheshimiwa.”n
29Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”o
30Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.”
31Lakini wao wakaondoka, wakaeneza habari za Yesu katika nchi ile yote.