Midvash

Matthew 22:2-14

2“Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.

3Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika.

4Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.

5Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake,

6na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua.

7Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.

8Kisha akawaambia watumishi wake: Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.

9Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje arusini.

10Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote, wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.

11“Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye hakuvaa mavazi ya arusi.a

12Mfalme akamwuliza, Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la arusi? Lakini yeye akakaa kimya.

13Hapo mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.”

14Yesu akamaliza kwa kusema, “Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa.”b

Copiado para área de transferência

Text Size

Aa

Reading Theme

Reading mode