Salmos 129
Mucho me han angustiado
Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: 2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. 3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.
4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. 5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. 6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”
¡Copiado!
Aa