Matthew 24:9-13
9“Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu.i
10Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
11Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.j
12Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.k
13Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka.l