Midvash

Matthew 1:20-23

20Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.d

21Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”e

22Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii:f

23“Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, naye ataitwa Emanueli” (maana yake, “Mungu yu pamoja nasi”).g

Copiado para área de transferência

Text Size

Aa

Reading Theme

Reading mode