Mark 13:33-37
33Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.h
34Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
35Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.i
36Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.
37Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!”