Midvash

John 18:2-8

2Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.

3Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.

4Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawauliza, “Mnamtafuta nani?”

5Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.

6Basi, Yesu alipowaambia: “Mimi ndiye”, wakarudi nyuma, wakaanguka chini.

7Yesu akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!”

8Yesu akawaambia, “Nimekwisha waambieni kwamba mimi ndiye. Basi, kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.”

Copiado para área de transferência

Text Size

Aa

Reading Theme

Reading mode